Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)

Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)

Kutoka kwa Huswain bin Abdirrahman amesema: Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa na Nge, akasema: nini ulifanya? nikasema: nilijisomea Ruqya, akasema: Ni nini kilikupelekea kufanya hivyo? Nikasema: Ni hadithi aliyotuhadithia Sha'abiy, akasema: Aliwahadithia nini? Nikasema: Alituhadithia kutoka kwa Buraida bin Huswaib yakwamba yeye amesema:"Hakuna kisomo cha ruqya isipokuwa kwa kijicho au homa", Akasema: Amefanya vizuri aliyeishia pale aliposikia, lakini alituhadithia sisi bin Abbasi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nilikusanyiwa mimi Ummati, nikamuona Nabii akiwa pamoja na kundi na Nabii akiwa pamoja na mtu mmoja na watu wawili, Na Nabii akiwa hana hata mtu mmoja, Ghafla ukanyanyuliwa kwangu weusi mkubwa, nikadhania kuwa hao ni umma wangu, nikaambiwa: Huyu ni Musa na watu wake, nikatazama tena, Ghafla nikaona weusi mkubwa, nikaambiwa: Huu ni umma wako, Ukiwa pamoja na watu elfu sabini wanaingia peponi bila hesabu wala adhabu, kisha akanyanyuka akaingia nyumbani kwake, watu wakazungumza mengi kuhusu watu hao (wanaoingia peponi bila hesabu wala adhabu); Wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliosuhubiana (walioambatana) na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliozaliwa katika uislamu na wakawa hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, Na wakataja mambo mengi! Basi akatoka kwao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakamueleza, Akasema: Hao ni wale ambao hawaombi watu kuwasomea ruqya, na wala hawajitibu kwa moto, na wala hawaamini mikosi ya ndege, na kwa Mola wao ndiko wanakotegemea, hapo akasimama (bwana mmoja akiitwa) Ukasha bin Mihswani akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, akasema: Wewe ni miongoni mwao, kisha akasimama mtu mwingine akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: kakutangulia kwa hilo Ukasha".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anatueleza Huswain bin Abdirrahman -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu mazungumzo yaliyojiri kati yake na Saidi bin Jubair -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu swala la kisomo cha Ruqya,Na hiyo ni kwasababu Huswain aling'atwa na nge na akajisomea kwaajili ya hilo ruqya ya kisheria, na alipomuuliza Saidi kuhusu ushahidi wake akamueleza kwa hadithi ya Sha'biy ambayo ina halalisha ruqya kwasababu ya kijicho au sumu,Saidi akamsifia kwa hilo,lakini yeye akampokelea hadithi ambayo inayopendekeza kuacha kufanya ruqya, nayo ni hadithi ya bin Abbasi ambayo inaambatana na sifa Nne ambazo atakayesifika nazo atastahiki kuingia peponi bila hesabu wala adhabu, nazo ni kutotafuta kisomo cha ruqya, na kutojitibu kwa moto,na kutoamini mikosi, na ukweli wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,na alipoomba Ukasha toka kwa Nabii-Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa amuombee ili awe miongoni mwao akamueleza kuwa yeye ni miongoni mwao,na aliposimama mtu mwingine kwa lengo hilo hilo akamjibu kwa upole Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kumzuilia hilo na kwa kufunga mlango na kukata muendelezo wa watu wengine.

التصنيفات

Ruq'ya ya Kisheria., Sifa za pepo na moto.