Hainifurahishi mimi kumiliki dhahabu mfano wa mlima huu wa Uhudi, zikapita siku tatu nikawa hata na dinari moja (katika mali hiyo) isipokuwa kiasi ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa deni, isipokuwa niseme kwa waja wa Mwenyezi Mungu hivi na vile.

Hainifurahishi mimi kumiliki dhahabu mfano wa mlima huu wa Uhudi, zikapita siku tatu nikawa hata na dinari moja (katika mali hiyo) isipokuwa kiasi ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa deni, isipokuwa niseme kwa waja wa Mwenyezi Mungu hivi na vile.

Kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ardhi yenye mawe katika mji wa Madina, tukaelekea mlima Uhudi, akasema: "Ewe Abuu Dhari" nikasema: Labbaika (nimekuitikia) Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Hainifurahishi mimi kumiliki dhahabu mfano wa mlima huu wa Uhudi, zikapita siku tatu nikawa hata na dinari moja (katika mali hiyo) isipokuwa kiasi ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa deni, isipokuwa niseme kwa waja wa Mwenyezi Mungu hivi na vile." akigeuka kuliani kwake na kushotoni kwake, na nyuma yake, kisha akatembea, Akasema: "Hakika wenye vingi ndio wenye vichache siku ya kiyama isipokuwa atakayezungumza kwa mali hivi na vile hivi na vile" akageuka kuliani kwake na kushotoni kwake na nyuma yake, "Na wachache katika wao" kisha akasema kuniambia "Bakia hapo usitoke mpaka nikujie" kisha akaondoka katika giza la usiku mpaka akapotelea, nikasikia sauti imenyanyuka, nikapata hofu isijekuwa kuna mtu kamvamia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- nikataka kumfuata nikakumbuka kauli yake "Bakia hapo usitoke mpaka nikujie" nikabakia mpaka aliponijia, nikasema: Nilisikia sauti nikaingiwa na hofu sana, nikamuelezea akasema: "Hivi uliisikia?" Nikasema: Ndiyo, akasema: "Huyo ni Jibril alinijia akasema: Atakayekufa katika umma wako hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi" Nikasema: Hata akizini na akaiba? Akasema: "Hata akizini na akaiba".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Maana ya hadithi: Anaeleza Abuu Dhari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akitembea na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ardhi yenye mawe katika mji wa Madina, ukawaelekea mlima wa Uhudi ambao unajulikana, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hainifurahishi mimi: Yaani hainipendezi mimi, kuwa mimi nina miliki dhahabu mfano wa mlima Uhudi na zikapata siku tatu hali yakuwa bado nina chochote katika mali hiyo, hata Dinari moja, isipokuwa kiasi nilichokiweka kwaajili ya kulipa deni, basi lau kama ningekuwa ninamiliki kiasi cha dhahabu halisi mfano wa mlima Uhudi basi ningekitoa chote katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nisingebakisha katika mali hiyo isipokuwa kile ninachohitajia kwaajili ya kulipa haki za watu, na kulipa madeni ninayodaiwa, na kisinge zidi chochote juu ya hayo, kwani mimi halinifurahishi kupita siku tatu hali yakuwa bado niko na mali hiyo. Na hii inaonyesha kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni mtu asiyekuwa na tamaa na dunia kuliko watu wote; kwasababu yeye hataki kukusanya mali isipokuwa ile anayoihifadhi kwaajili ya kulipa madeni, na alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa vazi lake la kivita kaliweka rehani kwa Yahudi kwasababu ya ngano aliyochukua kwaajili ya familia yake. Na lau kama dunia ingekuwa inapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnyima chochote Nabii wake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Dunia imelaaniwa na vimelaaniwa vilivyomo isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na vinavyofuata hilo, na mjuzi au mwenye kujifunza, na yale yote yanayokuwa katika utiifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema: "Wenye vingi ndio wenye vichache siku ya kiyama" Yaani wenye kuchuma vingi katika dunia ndio wenye matendo mema machache siku ya kiyama; kwasababu mara nyingi mtu zinapokithiri mali zake huwa anakuwa na hali ya kutosheka na kiburi na kupuuza mambo ya utiifu wa Mwenyezi Mungu; kwasababu dunia inampumbaza, anakua ni mwenye kutaka vingi duniani na kupungukiwa katika akhera. Na kauli yake: "isipokuwa atakayesema kwa mali hivi na vile hivi na vile" Yaani: Akazigawa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: "Na wachache katika wao" Na maana yake nikuwa wenye kutoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wachache. Kisha akasema: (Atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote ataingia peponi hata kama atazini na akaiba) Na hii haimaanishi kuwa zinaa na wizi ni mambo mepesi, bali ni mazito, na kwasababu hii aliyachukulia uzito Abuu Dhari na akasema: Hata kama atazini na akaiba? Akasema (Hata kama atazini na akaiba). Na hii ni kwakuwa atakayekufa katika imani na akawa na maasi katika madhambi makubwa; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hasemehe kushirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hilo kwa amtakaye" anaweza kumsamehe Mwenyezi Mungu wala asimuadhibu, na anaweza kumuadhibu, lakini hata akimuadhibu mwisho wake mafikio yake ni peponi; kwasababu kila aliyekuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na akawa hakufanya kitu kinachomtoa katika uislamu; basi mafikio yake ni peponi, ama atakayefanya linamuingiza katika ukafiri na akafa katika jambo hilo, huyu akabakishwa milele motoni na matendo yake yameporomoka; kwasababu wanafiki walikuwa wakisema kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- (Tunashuhudia kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu), na walikuwa wakimtaja Mwenyezi Mungu lakini hawamtaji Mwenyezi Mungu isipokuwa kidogo, na wanaswali lakini (Na wanaposimama katika swala husimama kwa uvivu) lakini pamoja na hiyo wao watakuwa katika tabaka la chini zaidi katika moto. Ikaonyesha juu ya kuipa nyongo (kuipuuza) dunia, nakuwa mwanadamu hatakiwi kuitundika nafsi yake katika dunia, na iwe dunia mkononi mwake na si moyoni mwake, mpaka moyo wake uelekee kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka; kwani huku ndiko kuipa nyongo dunia kikamilifu, Na haimaanishi kuwa usichukue chochote katika dunia; bali chukua katika dunia kilicho halali kwako, na wala usisahau fungu lako katika dunia, lakini iweke mkononi mwako na wala usiiweke moyoni mwako, Na hili ndilo la muhimu.

التصنيفات

Ubora wa Tauhiid.