Alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini

Alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akibakia msikitini akijitenga kwaajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu katika kila ramadhani siku kumi, na alikuwa akikaa itikafu katika siku kumi za katikati, kwa matarajio kuwa anaweza kuipata Lailatul Qadri (usiku wenye cheo), alipojua kuwa uko katika siku kumi za mwisho alikaa itikafu ndani ya siku hizo, kisha akakaa itikafu katika mwaka aliofishwa ndani yake siku ishirini kwa lengo la kuzidisha utiifu na kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Kufanya Itikafu.