Mchungeni(mfuatilieni) Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake

Mchungeni(mfuatilieni) Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake

Kutoka kwa Abuubakri Al-sswiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Mchungeni(mfuatilieni)Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake.

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Katika nukuu ya maneno ya Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuna ushahidi wa uelewa wa maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wa haki za watu wa familia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na kuwatukuza kwao na kuwaheshimu kwao, yeyote atakayekuwa ni katika watu wa familia yake na akawa kanyooka katika dini na mwenye kufuata sunna za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi huyo ana haki mbili: Haki ya uislamu na haki ya udugu wa karibu na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na nikuwa Abuubakari na maswahaba wengine walikuwa wakiwapenda watu wa nyumba ya Mtume na wakiusia kutendewa mazuri.

التصنيفات

Ubora wa watu wa nyumba ya mtume Radhi za Allah ziwe juu yao.