Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame

Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame

Kutoka kwa Abdallah bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Walishuhudia kwangu wanaume wanaoridhiwa -na ninaye mridhia zaidi kwangu ni Omar- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amekataza kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame" Na kutoka kwa Abuu Saidi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Hakuna swala baada ya sub-hi mpaka linyanyuke jua, na wala hakuna swala baada ya laasiri mpaka litoweke jua".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zake]

الشرح

Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hizi mbili kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua na linyanyuke toka msitari wa mawingu katika mtazamo wa macho kwa kiasi cha urefu wa mshale, na hili linaweza kukadiriwa kwa dakika kadhaa, wametofautiana wanachuoni katika kiwango chake, kuanzia dakika tano (5) mpaka kumi na tano (15). Na amekataza pia kuswali baada ya swala ya laasiri mpaka litoweke jua, kabla ya adhana ya magharibi kwa dakika chache; kwasababu katika kuswali ndani ya nyakati hizi kuna kujifananisha na washirikina wale wanaoliabudu wakati wa kuchomoza kwake na kuzama kwake, na tumekatazwa kujifananisha nao katika ibada zao; kwasababu atakayejifananisha na watu fulani basi nayeye ni miongoni mwao.

التصنيفات

Nyakati zilizo katazwa kusali.