Waliamrishwa watu kuwe kuagana kwao kwa mwisho ni katika nyumba (Alka'ba), isipokuwa likaondoshwa hilo kwa mwanamke mwenye hedhi

Waliamrishwa watu kuwe kuagana kwao kwa mwisho ni katika nyumba (Alka'ba), isipokuwa likaondoshwa hilo kwa mwanamke mwenye hedhi

Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema "Waliamrishwa watu kuwe kuagana kwao kwa mwisho ni katika nyumba (Alka'ba), isipokuwa likaondoshwa hilo kwa mwanamke mwenye hedhi".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Nyumba tukufu inaheshima na takrima; yenyewe ni alama ya ibada za Mwenyezi Mungu na utulivu na unyenyekevu mbele yake yeye, ikapata heshima ndani ya vifua, na utukufu ndani ya nyoyo, na mapenzi na kufungamana nayo. Na kwaajili hiyo akamuamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mwenye kuhiji iwe kuaga kwake ni hapo, na hii ndiyo twawafu (mzunguko) wa mwisho ambao ndio mzunguko wa kuaga, isipokuwa mwanamke mwenye hedhi; ni kwasababu huenda akauchafua msikiti kwa kuingia kwake, ikaondolewa kwake twawafu (mzunguko) bila kuufidia, na hii ni dalili katika hija hivyo haijumlishi na Umrah.

التصنيفات

Ubora wa uislamu na uzuri wake., Sifa za Hijjah.