Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza

Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza

Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba yeye alimuona mtu alishituka aliposikia mazungumzo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika sifa (za Allah) -akafanya kama ishara ya kulipinga hilo- akasema: "Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza".

[Sahihi] [Imepokelewa naIbn Abii A'swim - Imepokelewa na Abdul Razaaq]

الشرح

Anawakemea bin Abbasi watu miongoni mwa wale waliohudhuria kikao chake katika watu wa kawaida wanaopatwa na hofu pale wanaposikia chochote katika hadithi za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu sifa, na wanatikisika kama ishara ya kulipinga hilo, haijapatikana kwao imani ya wajibu kwa yale yaliyothibiti toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wakajua maana yake kutoka ndani ya Qur'ani ambayo muumini hawezi kuwa na shaka, na baadhi yao huzichukulia katika maana isiyokuwa yake aliyoitaka Mwenyezi Mungu wakaangamia kwa hilo.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Kitabu (Qur'an)