إعدادات العرض
Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu
Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu
Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහලالشرح
Maana ya hadithi: Nikuwa moto hautogusa jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo pindi anapokumbuka mtu ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya waja wake na uzembe wake katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu; akalia kwa kutaraji rehema zake na kuogopa adhabu zake na hasira zake, basi huyu kaahidiwa kusalimika na moto. Na jicho jingine ambalo moto hautoligusa, nalo ni: Yule atakayelala akilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu katika mipaka au sehemu ya mapigano kwa kuhifadhi roho za waislamu. Na kauli yake: "Hautoyagusa moto" Hii ni katika sehemu ya kutaja sehemu ya kitu na makusudio yake ni chote: nakuwa atakayelia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na atakayelala akilinda katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anaiharamisha miili yao katika moto.التصنيفات
Matendo ya moyoni.