Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku

Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku

Kutoka kwa Aisha na Abdillahi bin Omar na Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zote]

الشرح

Itakaposimamishwa swala, na chakula au kinywaji kikawa kiko tayari, inatakiwa kuanza na kula au kunywa mpaka yakatike matamanio ya mwenye kuswali, na akili yake asikaye anafikiria hilo, na aingie katika swala, na sharti ya hilo ni muda wa swala kutokuwa mfinyu, na uwepo wa uhitaji na kufikiria chakula, na hii inathibitisha ukamilifu wa sheria na kuzingatia kwake haki za nafsi pamoja na wepesi na upole.

التصنيفات

Adhana na Iqama.