Aliingia Abdur Rahmani bin Abiibakari As swiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mimi nikiwa nimemuegemeza kifuani kwangu, na Abdur Rahmani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa na mswaki mbichi akisukutua nao, akauelekezea Mtume -Rehema na…

Aliingia Abdur Rahmani bin Abiibakari As swiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mimi nikiwa nimemuegemeza kifuani kwangu, na Abdur Rahmani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa na mswaki mbichi akisukutua nao, akauelekezea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- macho yake-.

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Aliingia Abdur Rahmani bin Abiibakari As swiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mimi nikiwa nimemuegemeza kifuani kwangu, na Abdur Rahmani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa na mswaki mbichi akisukutua nao, akauelekezea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- macho yake-, nikauchukua mswaki nikautafuna, nikausafisha, kisha nikauelekeza kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akautumia kusukutua, sikuwahi kumuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisukutua kusukutua kuzuri kama kule, hakuchukua muda kumaliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: akanyanyua mkono wake na kidole chake, kisha akasema: kwa rafiki aliyejuu -kasema hivyo mara tatu- kisha akafariki, na alikuwa Aisha akisema: Amefariki baina ya tumbo langu na kidevu changu).

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kisa kinachotubainishia sisi kiwango cha mapenzi ya mswaki kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kushikamana kwake na mswaki, na hii nikuwa Abdur Rahman bin Abiibakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kaka yake na Aisha aliingia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa katika hali ya ulevi wa mauti. naye akiwa na mswaki mbichi, akisugua meno yake, alipouona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki ukiwa kwa Abdur Rahman, hayakumshughulisha yale aliyonayo katika maradhi na ulevi wa kifo, kwasababu ya mapenzi yake juu ya mswaki, akanyanyua macho yake kuutazama, kama mtu mwenye shauku nao, akagundua Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akauchukua mswaki toka kwa ndugu yake, na akakipunguza kichwa cha mswaki kwa meno yake, na akausafisha na kaupendezesha, kisha akampatia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akautumia kusukutua. Aliposafishika na akamaliza kupiga mswaki, alinyanyua kidole chake -akimpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na akichagua kuhamia kwa Mola wake Mtukufu, kisha akafariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akaweweseka, na ni haki yake kuwa hivyo, kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki na kichwa chake kikiwa juu ya kifua chake.

التصنيفات

Kufa kwake Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: