Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani…

Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani hujitenga mbali naye

Kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani hujitenga mbali naye". Ameongeza Abuudaudi: "Basi husema: -yaani shetani-: kuwaambia mashetani wengine: utaweza vipi kwa mtu aliyeongozwa na akatoshelezwa na akakingwa?".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Ameeleza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa mtu atakapotoka nyumbani kwake na akasema: Bismillaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu-, Tawakkalu a'lallaahi -Nimemtegemea Mwenyezi Mungu-, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahi- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Malaika humuita Ewe mja wa Mwenyezi Mungu umeongozwa katika njia ya haki, na umetoshelezwa mahitajio yako, na umehifadhiwa dhidi ya maadui; basi shetani aliyewakilishwa kwake hujitenga mbali naye, na hapo husema shetani mwingine kumwambia shetani huyu: utawezaje kumpoteza mtu tayari kaongozwa, na katoshelezwa, na amekingwa na mashetani wote? kwasababu yeye amesema maneno haya basi wewe hutomuweza.

التصنيفات

Adh-kaar za kutoka na kuingia nyumbani.