Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.

Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.

Kutoka kwa Sahli bin Sa'di Assaaidiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Katika hadithi kumebainishwa udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- nakuwa haina thamani, na lau ingekuwa hata na thamani ndogo zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnywesha kafiri hata funda moja ya maji, achilia mbali kule kuneemeka kwake nayo na kustareheka na mambo yake mazuri, Hivyo ikawa dunia ni dhalili mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tofauti na Akhera, kwani hiyo ni nyumba ya neema za kudumu kwa watu wenye imani na ni maalumu kwaajili yao kinyume na makafiri, hivyo inawapasa watu wenye imani wajue uhalisia wa hii dunia na wasiiegemee, kwani ni nyumba ya kupita na si nyumba ya kudumu, wachukue ndani yake yale yatakayowasidia Akhera ambayo ndiyo nyumba ya kudumu. Amesema Mtukufu: "Na hakuna chochote mlichopewa basi hicho ni starehe ya dunia na pambo lake, na yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ni yenye kubakia, hivi hamzingatii, hivi kwani tuliyemuahidi ahadi nzuri naye atakutana nayo anaweza kuwa sawa na tuliyemstarehesha starehe za maisha ya dunia kisha yeye siku ya kiyama atakuwa ni miongoni mwa wenye kuhudhurishwa".

التصنيفات

Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.