إعدادات العرض
1- Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama
2- Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake
3- Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.
4- Hakika kila umma una mtihani wake, na mtihani wa umma wangu: ni mali
5- Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni
6- Si chochote dunia katika Akhera isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu anapoweka kidole chake baharini, kisha atazame kimerudi na nini?
7- Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake
8- Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake
9- Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu
10- Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo
11- Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri
12- Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu
13- Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)
14- Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi
15- Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake
16- Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu
17- Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia
18- Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini ya mti kisha akaondoka akauacha
19- Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa