إعدادات العرض
Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu
Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu
Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français Kurdî Русский Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba lau kama mwanadamu angelipata bonde moja lililojaa dhahabu, basi angependa kwa sababu ya tamaa yake ambayo ndiyo maumbile yake awe na mabonde mengine mawili, na kwamba mwanadamu haachi kuipupia dunia mpaka anakufa na lijae tumbo lake kwa udongo wa kaburi lake.فوائد الحديث
Pupa kubwa ya mwanadamu ya kukusanya mali na vinginevyo katika starehe za Dunia.
Amesema Nawawi: Hapa kumekemewa pupa ya kuipupia Dunia na kupenda wingi wa mali na kuwa na tamaa.
Mwenyezi Mungu anaikubali toba ya mwenye kutubia kutokana na sifa mbaya.
Amesema Nawawi: Hadithi imekuja katika mfumo wa kueleza hali ya wanadamu wengi katika kuipupia Dunia, na inaungwa mkono na kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Na Mwenyezi Mungu humsamehe mwenye kuomba msamaha".