إعدادات العرض
Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia
Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia".
[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Hausa Kurdî Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Românăالشرح
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kujitengenezea makonde na mabustani na mashamba; kwa sababu hilo ni katika sababu za kuipenda sana dunia na kubweteka nayo na kuisahau Akhera.فوائد الحديث
Katazo la kukithirisha sana hadhi za kidunia kwa sababu hupelekea kuiacha Akhera.
Katika hadithi hakuna katazo la kutengeneza yale yanayopelekea maisha, bali katazo ni kuzama katika dunia na kuisahau Akhera.
Amesema Sanadi: Na makusudio yake: Nikuwa msizame katika kutengeneza mabustani, mkapumbazika nayo na mkajisahau kumtaja Mwenyezi Mungu.