Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake

Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba siku moja Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikaa juu ya Mimbari na tukakaa pembezoni mwake, akasema: "Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi kheri inaweza kuleta shari? Akanyamaza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakamwambia: Una nini wewe? Unamsemesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wala hakusemeshi? Tukamuona akiteremshiwa wahyi, anasema: akafuta jasho, akasema: "Yuko wapi muulizaji?" ni kana kwamba alipendezwa na swali lake, akasema: "Hakika kheri haileti shari, na hakika katika yale yanayooteshwa na masika huua au kudhuru, isipokuwa mifugo wanaokula malisho ya kijani, hula mpaka zinapopanuka mbavu zao hulielekea Jua, hujisaidia haja kubwa na ndogo, na wakapumzika, na hakika mali hii ni kijani kitamu, neema bora ya mtu muislamu ni ile aliyoitoa kumpa masikini na yatima na mpita njia -Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake- na hakika atakayeichukua pasina haki yake, ni sawa na yule anayekula wala hashibi na atakuwa shahidi juu ya mali hiyo siku ya Kiyama".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikaa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja juu Mimbari akiwahadithia Maswahaba zake akasema: Hakika kikubwa ninachokihofia zaidi kwenu nyinyi baada yangu ni yale mtakayofunguliwa katika baraka za Ardhi na maua ya Dunia na pambo lake, na muonekano wake, na yale yaliyomo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na nguo na mazao na mengineyo miongoni mwa yale ambayo watu hujifaharisha kutokana na uzuri wake pamoja nakuwa yanadumu kwa muda mchache. Mtu mmoja akasema: Maua ya Dunia ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, je inaweza kurudi neema hii na kuwa janga na adhabu?! Watu wakamlaumu muulizaji pale walipomuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake kanyamaza, na wakadhania kuwa kamkasirisha. Ikabainika kuwa rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiteremshiwa wahyi, kisha akaanza kufuta jasho katika paji lake la uso, akasema: Yuko wapi muulizaji? Akasema: Mimi. Akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kheri ya kweli haiji ila kwa kheri, lakini maua haya si kheri halisi kwa kuwa yanapelekea katika fitina na kushindana na kushughulika nayo na kuwacha kuielekea Akhera kikamilifu, kisha akapigia mfano wa hilo akasema: Hakika mimea ya masika na kijani chake; nayo ni aina za mimea ambazo huwapendeza sana wanyama, na huwaua kwa kuila kwa wingi na kuvimbewa au hukaribia kuwaua, isipokuwa mnyama anayekula mimea ya kijani aliyekula mpaka ikajaa sehemu ya tumbo lake, akaelekea juani na akatoa kinyesi chepesi kutoka tumboni mwake au akakojoa, kisha akayacheua yaliyoko tumboni mwake kisha akayatafuna kisha akayameza, kisha akarudi kula tena. Hivyo mali hii ni kama majani ya kijani matamu, yanaua au yanakaribia kuuwa yanapokithiri; isipokuwa kama atatosheka na kidogo ambacho anahaja nacho na kitakachomtosha kwa njia ya halali, hii haidhuru, na neema bora ya muislamu ni kwa yule atakayetoa na kumpa masikini na yatima na mpitanjia, na yule mwenye kuichukua kwa haki atakabarikiwa katika mali hiyo, na atakayeichukua pasina haki yake mfano wake ni kama mfano wa yule anayekula wala hashibi, na mali hiyo itakuwa shahidi juu yake siku ya Kiyama.

فوائد الحديث

Amesema Nawawi: Ndani yake kuna: Ubora wa mali kwa yule atakayeichukua kwa haki yake na kuitoa katika njia za kheri.

Kaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hali za umma wake, na yale watakayofunguliwa katika mapambo ya maisha ya dunia na fitina zake.

Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kupiga mifano ili kuleta karibu maana.

Himizo la sadaka na kuitoa mali katika njia za kheri, na tahadhari ya kuizuia.

Inachukuliwa kutoka katika kauli yake: "Hakika kheri haileti shari" Kuwa riziki hata ikiwa nyingi ni miongoni mwa kheri, bali hujitokeza shari kwa sababu ya kujitokeza ubahili kwa yule mwenye kustahiki kupewa, na kufanya ubadhirifu kwa kuitoa katika mambo yasiyotakiwa, nakuwa kila kitu alichokihukumu Mwenyezi Mungu kuwa kheri hakiwezi kuwa shari na kinyume chake pia, lakini inahofiwa kwa yule atakayeruzukiwa kheri huenda yakajitokeza katika matumizi yake mambo yanayomletea shari.

Kuacha haraka ya kujibu ikiwa jambo linahitaji kuzingatiwa.

Amesema Attwayibi: Inachukuliwa kutoka katika hadithi hii makundi manne: Atakayekula kutoka katika mali hiyo ulaji wa mtu mwenye kutaka starehe za kupitiliza tena mwenye kuzama ndani ya starehe mpaka zikavimba mbavu zake na akaendelea basi huyu maangamivu yatamfika haraka, na atakayekula vile vile lakini akatumia ujanja kwa ajili ya kuondoa maradhi baada ya kumsumbua kwa muda mrefu lakini akazidisha itamuangamiza, na atakayekula vile vile lakini akafanya haraka kuondoa yanayomdhuru na akayamaliza mpaka chakula chake kikawa sawa kwa kumeng'enywa pasina kuzidisha basi huyu atasalimika, na atakayekula pasina kupita kiasi wala ulafi, bali akaishia katika yale yanayoziba njaa yake na kuzuia kiu yake, mtu wa kwanza ni mfano wa kafiri, na wa pili ni mfano mtu aliyeasi na kughafilika kutoacha na kufanya toba ila baada ya kupitwa na wakati, na wa tatu ni mfano wa mtu mwenye kuchanganya mazuri na mabaya mwenye kwenda mbio kufanya toba kiasi ambacho toba yake hukubalika, na wanne ni mfano wa mtu aliyeipa nyongo dunia mwenye tamaa na Akhera.

Amesema bin Munir: Katika hadithi hii kuna namna za kufananisha za kielimu, ya kwanza: Kufananisha mali na kudhihiri kwake na kukua kwake na mimea, ya pili: Kumfananisha anayezama katika kuichuma na sababu za kuipata na wanyama wanaopupia malisho, na ya tatu: Kufananisha kuikithirisha kwake na kuilimbikiza na tumbo linapokula na kujaa, na ya nnne: Kufananisha mali inayotoka pamoja nakuwa ni ngumu katika nafsi mpaka ikapelekea katika ubahili uliopitiliza na kile wanachokitoa wanyama katika uchafu, hapa kuna ishara ya hali ya juu sana kuwa sheria imeiona kama uchafu, na ya tano: Kumfananisha aliyebweteka baada ya kuikusanya na mbuzi anapostarehe na akaweka mwili wake juani; kwani hapo ni katika sehemu zake nzuri ambazo hupata utulivu, na pia kuna ishara ya kuitumia mali hiyo kwa maslahi mazuri, na ya sita: Kufananisha kifo cha mwenye kukusanya mali na kutoitoa, na kifo cha mnyama alighafilika na kuzuia yale yanayomdhuru, ya saba: Ni kuifananisha mali na rafiki ambaye haaminiki huenda akageuka kuwa adui; kwa sababu tabia ya mali ni kulindwa na kuhifadhiwa kwa sababu ya kupendwa na watu; na hilo linapelekea kuizuia na kutompa mwenye kustahiki ndio inakuwa sababu ya kuadhibiwa mmiliki wake, na ya nane: Ni kumfananisha mwenye kuichukua pasina haki na anayekula pasina kushiba.

Amesema As-Sanadi: Kheri ni lazima iwe na mambo mawili, la kwanza: Kuipata kwa njia zake sahihi, na la pili: Kuitoa katika matumizi sahihi, na linapokosekana moja wapo basi inageuka nakuwa madhara... na inaweza kusemwa: Hapa kuna ishara ya kushikamana na vigezo viwili hivyo; na mtu hawezi kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu kuitumia katika njia sahihi isipokuwa akiichuma kwa njia za halali.

التصنيفات

Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.