Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama

Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama

Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu wanaotumia mali ya waislamu kwa batili, na wanaichukua pasina haki, na maana hii inajumuisha kuanzia ukusanyaji wake, na uchumaji wake bila uhalali wake, na utoaji wake katika sehemu zisizo sahihi, na inaingia katika hilo kula mali ya yatima na mali ya wakfu, na kutotunza amana, na kuchukua chochote katika mali ya umma bila ya haki. Ameeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo yao ni moto siku ya Kiyama.

فوائد الحديث

Mali iliyoko mikononi mwa watu ni mali ya Mwenyezi Mungu, amewamilikisha ili waitoe katika njia za kisheria, na waepuke kuitumia katika batili, na hii inawahusu viongozi na wasiokuwa viongozi.

Sheria imetia mkazo katika mali ya umma, nakuwa yeyote atakayesimamia chochote basi atambue kuwa atahesabiwa juu ya ukusanyaji wake na matumizi yake.

Anaingia katika ahadi hii ya adhabu mwenye kufanya matumizi yasiyokuwa ya kisheria katika mali, sawa sawa iwe ni mali yake, au mali ya mwingine.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.