إعدادات العرض
Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake
Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Kinyarwanda Română తెలుగు Lietuvių Oromoo മലയാളം Nederlands Soomaali Shqip Српски Deutsch Українська ಕನ್ನಡ Wolofالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia ina ladha tamu, na ni kijani katika mandhari, hivyo mwanadamu hudanganyika nayo na kuikimbilia na kuifanya kuwa ndio hamu yake kubwa. Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafanya baadhi yetu kuwa warithi wa wengine katika dunia hii, ili aone ni namna gani tutafanya, je tutasimama katika utiifu wake, au maasi yake? Kisha akasema: Tahadharini sana na zisikudanganyeni starehe za Dunia na mapambo yake, zikakupelekeeni kuacha aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu, na kuingia katika yale aliyokukatazeni. Na miongoni mwa mambo makubwa ya wajibu kutahadhari nayo katika fitina za Dunia ni fitina ya wanawake, nakuwa ndio iliyokuwa fitina ya kwanza waliotumbukia ndani yake wana wa Israeli.فوائد الحديث
Himizo la kushikamana na uchamungu, na kutojishughulisha na mambo ya kidunia na pambo lake.
Tahadhari ya kufitinika na wanawake, kwa kuwatazama au kujiachia kwa kuchanganyika na wanaume wa kando, au mengineyo.
Fitina ya wanawake ni katika fitina kubwa katika Dunia.
Kuzingatia na kuchukua mafunzo kutoka katika umma zilizotangulia, kilichotokea kwa wana wa Israeli kinaweza kutokea kwa wengine pia.
Fitina ya wanawake, akiwa ni mke anaweza kumbebesha mwanaume mzigo mkubwa wa matumizi asiouweza, na akamshughulisha na kutafuta mambo ya kidunia, na akampelekea kumaliza umri wake katika kuitafuta Dunia, na akiwa ni mwanamke wa kando, anaweza kumfitini kwa kumlaghai mwanaume na kumtoa katika haki pale wanawake wakitoka na kuchanganyika pamoja na wanaume, hasa hasa wakiwa hawajisitiri kisheria, na hili linaweza kupelekea kuingia katika zinaa kwa ngazi zake, hivyo ni lazima kwa muumini kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na kuelekea kwake ili kusalimika na fitina za zao.