إعدادات العرض
Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa
Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -radhi za Allah ziwe juu yao wawili ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlands አማርኛ Hausa සිංහලالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba amefaulu na amebahatika atakayemtii Mola wake akaongozwa na akawezeshwa kuingia katika Uislamu, na akaruzukiwa katika halali kiasi cha mahitaji yake pasina ziada wala mapungufu, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kukinai na kuridhika na kile alichompa.فوائد الحديث
Utukufu wa mtu upo katika ukamilifu wa dini yake na kupata cha kumtosheleza katika maisha yake na kutosheka kwake na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu.
Himizo la kutosheka kwa kile ulichopewa katika dunia ikiwa ni pamoja na Uislamu na sunna.