إعدادات العرض
Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende
Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Bahasa Indonesiaالشرح
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.فوائد الحديث
Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama vile kuipa nyongo dunia na kuzipuuza ladha za dunia, pamnoja nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa uwezo wa hilo lau kama angetaka kustarehe nayo.
Inafaa kutumia magodoro na mito, na kuvilalia na kuwa juu yake.
Muislamu anatakiwa kuzingatia hali yake na hali ya maisha ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake. Kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba mwenye kuiga nyenendo zake ataongoka na atafaulu duniani na Akhera.
Kuwa na pupa ya kuiandaa Akhera, na muumini atosheke katika dunia na kile kinachomsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, na asishughulike na kutafuta wingi wa mali ndani yake, na aliwakemea Mwenyezi Mungu watu, akasema: "Kumekupumbazeni kutafuta wingi (wa mali) mpaka mkayazuru makaburi" [Takathur: 1-2].
