إعدادات العرض
1- Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kukimpendeza sana kuanzia kulia katika kuvaa kwake viatu, na kuchana kwake nywele, na kujisafisha kwake, na katika mambo yake yote.
2- Nilisali pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- rakaa mbili kabla ya adhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Ijumaa, na rakaa mbili baada ya magharibi, na rakaa mbili baada ya ishaa
3- Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki
4- Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri.
5- Yakwamba Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa safarini, akaswali swala ya ishaa ya mwisho, akasoma katika moja ya rakaa mbili kwa sura ya wattin wazzaitun, sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri au kisomo kizuri zaidi yake
6- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa lake
7- Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na pia kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili
8- Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba