إعدادات العرض
Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka
Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka
Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Bahasa Indonesiaالشرح
Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.فوائد الحديث
Manabii hawarithiwi.
Kumebainishwa alivyoviacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada ya kifo chake.
Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha kitu chochote cha msingi, kutokana na ukarimu wake na utoaji wake na wema wake.
Amesema Al-Karmani: Dhamiri katika kauli yake "na akavifanya" hii inarudi katika vitu vitatu: Yaani; nyumbu na silaha na Ardhi na si katika Ardhi peke yake.
Shemeji: Ni kaka wa dada, na neno "Akhtani" hutumika kwa ndugu wa mwanamke.
