Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki

Kutoka kwa Hudhaifa bin Yamani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Katika mapenzi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake ya usafi na kuchukia kwake harufu mbaya nikuwa yeye alikuwa anapoamka kutoka katika usingizi mrefu ambao ndio unadhaniwa kuwa sababu ya kubadilika kwa harufu ya mdomo, alikuwa akisugua meno yake -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa mswaki, ili akate harufu mbaya, na ili achangamke baada ya usingizi kuzidi kusimama kwake; kwasababu katika mambo maalumu kwa mswaki pia ni kuzindua na kuchangamsha.

التصنيفات

Sunna za Kimaumbile., Muongozo wa Mtume Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani katika kujitwaharisha.