Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi

Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi

Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zote]

الشرح

Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.

فوائد الحديث

Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.

Sheria ya kuswali sunna nyumbani.

التصنيفات

Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu., Muongozo wake Mtume Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani katika swala, Muongozo wake Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani katika Ndoa na kuamiliana na wake zake.