إعدادات العرض
Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki
Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands Bahasa Indonesia ਪੰਜਾਬੀالشرح
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.فوائد الحديث
Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya maisha ya chini, kwani maisha halisi ni maisha ya Akhera.
Amesema bin Hajari: Na kinachoonekana nikuwa sababu ya kutoshiba kwao mara nyingi ilikuwa ni kwa sababu ya uchache wa upatikanaji wa chochote kwao, yaani walikuwa wakipata chakula lakini walikuwa wakithamini wenye shida zaidi yao kuliko nafsi zao.
