Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa…

Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri.

Kutoka kwa Zainab bint Jahshi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliingia kwake akiwa na hali ya mfadhaiko, akisema: "Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Kutoka kwa mama wa waumini Zainab binti Jahshi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliingia kwake hali uso wake ukiwa mwekundu, akisema: "Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu" akiithibitisha tauhidi na akiituliza nafsi. kisha akawatahadharisha waarabu akasema: Ole wao waarabu, kutokana na shari iliyokaribia", kisha akabainisha kuwa shari hii nikuwa imefunguliwa nafasi ndogo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-ajuju, kwa kiasi cha mduara uliyoko baina ya vidole viwili kidole cha shahada na kidole gumba. Akasema Zainab: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Je, hivi tunaweza kuangamia hali yakuwa miongoni mwetu kuna watu wema?, Akaeleza kuwa mwema haangamii, bali yeye ni mwenye kusalimika mwenye kuokoka; lakini machafu yakikithiri na mwema pia anaangamia, yatakapokithiri matendo machafu mabaya katika jamii hata kama watakuwa ni waislamu na yakawa hayakukemewa, basi wao watakuwa wamezitia nafsi zao katika maangamivu.

التصنيفات

Alama za Kiama ., Muongozo wake Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani katika Ndoa na kuamiliana na wake zake.