"Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami

"Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Lilikuja kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, katika nyumba za wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakiuliza kuhusu ibada zake za siri ndani ya nyumba yake, walipoelezwa wakawa kana kwamba za kwao wameziona ndogo, wakasema: Na tuko wapi sisi na Mtume rehema na amani ziwe juu yake? hali yakuwa amekwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, ukilinganisha na ambaye hajajua hata kupatikana kwa msamaha, huyu anahitaji kupitiliza katika kufanya ibada huenda akaupata msamaha huo. Kisha wakasema baadhi yao: Sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala katika godoro. Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akachukia, na akawahutubia watu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, na akasema: Wana nini watu fulani waliosema kadhaa wa kadhaa?! Wallahi mimi ndiye ninayemuhofu sana Mwenyezi Mungu kuliko watu wote na ndiyo mchamungu wenu, lakini ninalala ili nipate nguvu ya kusimama, na ninafungua ili nipate nguvu ya kufunga, na ninaoa wanawake, atakayeipuuza njia yangu, na akaona njia nyingine ndio iliyokamilika, na akachukua njia ya asiyekuwa mimi, huyu hayuko nami.

فوائد الحديث

Mapenzi ya kheri kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na shauku yao juu yake, na kwa baadhi yao kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Upole wa sheria hii na wepesi wake, kwa kuchukua kutoka katika matendo ya Nabii wao na muongozo wake.

Kheri na baraka iko katika kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kufuata hali zake tukufu.

Kemeo la kuitilia mkazo nafsi katika ibada kwa yale isiyoyaweza, nakuwa hili ni katika hali za wazushi.

Amesema bin Hajari: Kuchukua kwa mkazo katika ibada kunapelekea katika uchovu unaokata asili yake, na kudumu na kuishia katika faradhi peke yake, na kuacha kufanya sunna kunapelekea kuamsha uvivu, na kukosa uchangamfu katika ibada, na jambo bora ni la kati na kati.

Hapa kuna fundisho la kufuatilia hali za wakubwa kwa ajili kuiga kutoka katika matendo yao, nakuwa inaposhindikana kulijua hilo kutoka kwa wanaume inafaa kulibaini hilo kutoka kwa wanawake.

Hapa kuna mawaidha na kutoa maswala ya kielemu na kubainisha hukumu kwa watu wazima, na kuondoa utata kwa wale wenye kujitahidi.

Amri ya kujihurumia katika ibada, ikiwa ni pamoja na kuihifadhi na kuzihifadhi faradhi na sunna; ili muislamu achunge haki za mtu mwingine.

Katika hadithi kuna dalili juu ya fadhila za ndoa na himizo lake.

التصنيفات

Muongozo wa Mtume.