إعدادات العرض
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Português Kurdî Magyar ქართული Românăالشرح
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.فوائد الحديث
Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.