إعدادات العرض
1- Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo.
2- Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake
3- Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.
4- Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea.
5- Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike.