Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume)

Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia mahali ambapo atakidhi haja yake hapo, haja ndogo au kubwa, anaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu, na anajielekeza kwake amkinge na shari za mashetani wa kiume na wa kike, Na limetafsiriwa neno khubuthi na khabaaithi (Mashetani wa kiume na wa kike) kwa maana ya shari na najisi.

فوائد الحديث

Sunna ya dua hii wakati wa kutaka kuingia msalani.

Viumbe wote ni wahitaji kwa Mola wao Mlezi katika kuzuia yenye kuwaudhi au kuwadhuru katika hali zao zote.

التصنيفات

Adabu ya Kukidhi Haja.