Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.

Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.

Kutoka kwa Abuu Ayyub Al-answariy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi". Akasema Abuu Ayyub: "Tukaenda sham, tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea upande wa kibla, tukawa tunapinda, na tunamuomba Mwenyezi Mungu msamaha".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaelekeza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika kitu miongoni mwa adabu za kukidhi haja kuwa wasielekee kibla, nayo ni Al-ka'aba tukufu, na wala wasikipe mgongo wakati wa kukidhi haja; kwasababu ndio uelekeo wa swala, na ni mahala pa kutukuzwa na kupaheshimu, na wanatakiwa wapinde waelekee upande wa mashariki au magharibi itakapokuwa upande wa mashariki au magharibi hauelekei huko, kama kibla cha watu wa Madina. Na kwakuwa Maswahaba ndio watu wepesi zaidi kukubali amri ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, ambayo ndiyo haki, ameeleza Abuu Ayyub kuwa wao walipokwenda Sham baada ya Fat-hi (Ufunguzi wa mji wa Makka) wakakuta huko vyoo vilivyoandaliwa kwaajili ya kukidhi haja, vimejengwa kwa kuelekea kibla, wakawa wanapinda kibla, na wanaomba msamaha kwasababu ya unyenyekevu na tahadhari.

التصنيفات

Kuondoa Najisi., Kuondoa Najisi., Adabu ya Kukidhi Haja., Adabu ya Kukidhi Haja.