إعدادات العرض
1- Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.
2- Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
3- Nilikuwa ni mtu mwenye madhii mengi, nikaona haya kumuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu ya nafasi ya binti yake kwangu, nikamtuma Mikidadi bin Aswadi akamuuliza, akasema: Ataosha tupu yake, na atatawadha