Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha

Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha

Kutoka kwa Ummu Qais bint Mihswan -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuja mama Kaisi binti Mihswan radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake hajaanza kula chakula kutokana na udogo wa umri wake, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, mtoto akakojoa katika nguo yake rehema na amani ziwe juu yake, akaomba maji, na akanyunyiza katika nguo yake na wala hakuiosha.

فوائد الحديث

Tabia njema za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na unyenyekevu wake wa hali ya juu.

Wito wa kuishi vizuri na watu na unyenyekevu na upole kwa watoto, na kulea nyoyo za watu wazima kwa kuwakirimu watoto wao na kuwakalisha mapajani, na mfano wa hayo.

Najisi ya mkojo wa mtoto mdogo hata asipokula chakula kwa matamanio.

Kitendo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kinaitwa kunyunyiza, hicho ni maalumu kwa mtoto mdogo wa kiume ambaye hajaanza kula chakula, ama mtoto wa kike ni lazima kuosha mkojo wake hata akiwa mdogo.

Kinyesi cha mtoto wa kiume ambaye chakula chake ni maziwa ya mama yake ni lazima kuosha kama najisi zingine.

Kuosha ni lazima kuwe na jambo la ziada kama kufikisha maji.

Kilicho bora ni kufanya haraka kusafisha mahali palipo na najisi; ili kufanya haraka kujitwaharisha kutokana na uchafu; na ili asisahau.

التصنيفات

Kuondoa Najisi.