إعدادات العرض
Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe
Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe
Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Kinyarwanda తెలుగు Lietuvių Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali Српски Українська Deutsch ಕನ್ನಡ Wolof Moore Shqip ქართული Azərbaycan Magyar தமிழ் Македонскиالشرح
Ameeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka katika tupu wakati wa matamanio au kabla ya tendo ya ndoa-, Na wala hajui afanye nini yakitoka, akaona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu yeye ni mume wa Fatma binti wa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Akamuomba Mikidadi bin Aswadi amuulize Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhuus hilo, Basi akajibu Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa aoshe tupu yake kisha atawadhe.فوائد الحديث
Ubora wa Ally bin Abi Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi ambacho haya haikumzuia kuacha kuuliza kupitia mtu mwingine.
Inafaa kutuma mtu kwa niaba kwa ajili ya kuuliza.
Inafaa kumueleza mtu mambo binafsi kwa sababu ya kuona haya ikiwa kuna masilahi.
Unajisi wa madhii, na uwajibu wa kuyaosha katika mwili na nguo.
Kutoka kwa madhii ni katika vitenguzi vya udhu.
Uwajibu wa kuosha utupu na korodani mbili kwa kuwa zimetajwa katika hadithi nyingine.
التصنيفات
Kuondoa Najisi.