إعدادات العرض
Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tagalog ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල አማርኛ অসমীয়া ગુજરાતી Tiếng Việt Nederlands नेपाली پښتو ไทย Svenska മലയാളം Кыргызча Română తెలుగు Malagasyالشرح
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake chombo hicho kioshwe mara saba ikiwa mbwa ataingiza ulimi wake ndani yake, mara ya kwanza iwe kwa mchanga, ili yaje maji baada yake, hivyo usafi kamili utakuwa umepatikana kutokana na najisi yake na madhara yake.فوائد الحديث
Mate ya mbwa ni najisi tena ni najisi nzito.
Mbwa kulamba katika chombo, kunakitia najisi chombo hicho, na kunanajisisha maji yaliyoko ndani yake.
Kusafisha kwa udongo na kurudia mara saba hii ni maalum kwa kusafisha pale atakapo lamba, lakini si katika mkojo wake na uchafu wake na vyote atakavyovichafua mbwa.
Jinsi ya kuosha chombo kwa udongo: Ataweka maji ndani ya chombo na kuongeza udongo ndani yake, kisha atasafisha chombo kwa mchanganyiko huu.
Maana ya dhahiri ya Hadith ni kuwa hadithi hii inajumuisha mbwa wote, hata mbwa ambao sheria imeruhusu kufugwa, kama vile kuwinda, kulinda, na mbwa wa mifugo.
Sabuni na majani ya miti havichukui nafasi ya udongo; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliweka sharti la kutumia udongo.