Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.

[Sahihi]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotoka kukidhi haja yake msalani anasema: " Ninakuomba (Msamaha) Ewe Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Ni sunna kusema: "Ghufraanaka" baada ya kutoka mahala pa kukidhi haja.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumtaka msamaha Mola wake katika hali zake zote.

Inasemekana katika sababu ya kuomba msamaha baada ya kukidhi haja ni kwa sababu ya uzembe wa kushukuru neema nyingi za Mwenyezi Mungu, ikiwemo kurahisishiwa kutoka kile kinachokuudhi, na ninaomba msamaha wako kwa kushughulishwa na kukidhi haja nikaacha kukutaja.

التصنيفات

Adabu ya Kukidhi Haja.