Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi

Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi

Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi, na alikuwa akitoa kichwa chake kwangu, naye akiwa katika itikafu (msikitini), ninamuosha nami nikiwa katika hedhi".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu baadhi ya hali zake maalum pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwake: Nikuwa alikuwa akioga kutokana na janaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja wakichota wote kwa pamoja. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumwendea akiwa katika hedhi anamuamrisha afunike mwili wake kuanzia kitovuni mpaka magotini, kisha akimshikashika bila ya tendo la ndoa. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu msikitini anatoa kichwa chake kwa Aisha anamuosha naye akiwa nyumbani kwake na akiwa katika siku zake.

فوائد الحديث

Inafaa mtu kuoga na mke wake katika chombo kimoja.

Inafaa kumpapasa mwenye hedhi, mahali pasipokuwa tupu, nakuwa mwili wake ni twahara na wala si najisi.

Inapendeza kwa mwanamke kuvaa kikoi (au mtandio) wakati wa kupapaswa.

Kuchukua sababu zinazozuia kuingia katika haramu.

Katazo kwa mwenye hedhi kukaa msikitini.

Uhalali kwake wa kuvipapasa vitu vibichi au vikavu, ikiwemo kuziosha nywele na kuzitana

Muamala mzuri wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa familia yake.

التصنيفات

Muongozo wake Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani katika Ndoa na kuamiliana na wake zake.