Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri

Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.

فوائد الحديث

Amesema Nawawi: Kila muumini ni mfungwa, amezuiliwa katika dunia kuyaendea matamanio yaliyoharamishwa pamoja na machukizo, amelazimishwa kufanya matendo ya utiifu na magumu, basi akifa anapumzika na haya, na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa neema za kudumu, na raha halisi isiyokuwa na mapungufu, na ama Kafiri basi yeye huyamiliki hayo aliyoyapata katika starehe za dunia, pamoja nakuwa ni machache, na yamejawa tabu ziilizojaa vikwazo mbali mbali, hivyo, anapokufa anaingia katika adhabu ya kudumu, na mateso ya milele.

Amesema Assanadi: Kauli yake: "Gereza la Muumini" Bila shaka hata kama ndani yake kuna neema, basi Pepo ni bora kwake kuliko hizo, "Na Pepo ya Kafiri" Basi hata kama kuna machukizo ila Moto ndio shari zaidi kwake kuliko hayo.

Udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Dunia ni nyumba ya majaribu na mitihani kwa wenye imani.

Kafiri ameiwahisha Pepo yake Duniani; akaadhibiwa kwa kunyimwa Pepo Akhera na neema zake.

التصنيفات

Kuipa nyongo Dunia na Kujiepusha na yaliyo haramu., Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.