Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo

Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo.

[Ni nzuri]

الشرح

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kukithirisha kukikumbuka kifo ambacho kukikumbuka kwake mtu anakumbuka Akhera, na kunabomoa mapenzi yake ya kupenda ladha za dunia ndani ya moyo wake, na hasa hasa zile za haramu.

فوائد الحديث

Kifo kinakata ladha za dunia, lakini kwa muumini kinamuhamisha kwenda katika ladha za Akhera na ladha za pepo na yale yanayopatikana ndani yake miongoni mwa kheri kubwa.

Kukumbuka kifo na yale yanayokuwa baada yake ni miongoni mwa sababu za kutubia na kujiondoa katika dhambi na kujiandaa na Akhera.

التصنيفات

Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.