إعدادات العرض
Waelezeni watu yale wanayoyafahamu, Hivi mnataka akadhibishwe (apingwe) Mwenyezi Mungu na Mtume wake
Waelezeni watu yale wanayoyafahamu, Hivi mnataka akadhibishwe (apingwe) Mwenyezi Mungu na Mtume wake
Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Waelezeni watu yale wanayoyafahamu, Hivi mnataka akadhibishwe (apingwe) Mwenyezi Mungu na Mtume wake?".
[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහලالشرح
Anaelekeza Kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa haitakiwa watu wote kuelezwa isipokuwa yale mambo ambayo ni maarufu tena yenye kuwanufaisha watu katika msingi wa dini yake na hukumu yake miongoni mwa tauhidi na kuwabainishia watu halali na haramu, na kuacha yenye kupoteza lengo hilo; katika yale yasiyokuwa na haja ndani yake, au yakawa ni katika mambo ambayo ni sababu ya kupingwa ukweli na kutokubalika kwake katika yale ambayo wanatatizika kuyafahamu, na inakuwa kwao vigumu kuyajua.التصنيفات
Kulingania na kuelekeza kwa Mungu.