Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu

Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu

Kutoka kwa Abdillah bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu".

[Albany amenukuu usahihi wake kutoka kwa Ibn Taymiyyah na hakuifatilia] [Imepokelewa na Ibnu Jariri - Imepokelewa na Adh-dhahaby katika kitabu cha Uluwwi - Imepokelewa na Abdallah bin Al-Imam Ahmad]

الشرح

Anatueleza Abdillahi bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika nukuu hii kuwa kiwango cha asilimia ya mbingu saba na ardhi saba pamoja na ukubwa wake katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa Rehema-, ni kama kiwango cha punje ndogo ya ulezi katika kiganja cha mmoja wetu, na hii ni kufananisha kiwango kwa kiwango, na si kufananisha kiganja kwa kiganja; kwasababu Mwenyezi Mungu sifa zake hazifanani na kitu chochote kama ambavyo dhati yake haifanani na chochote.

التصنيفات

Kumuamini Allah mwenye nguvu alie tukuka