إعدادات العرض
Ni nani anayejiapiza kwangu kuwa sitomsamehe fulani? Hakika mimi nimemsamehe,na nimeyaporomosha matendo yako
Ni nani anayejiapiza kwangu kuwa sitomsamehe fulani? Hakika mimi nimemsamehe,na nimeyaporomosha matendo yako
Kutoka kwa Jundabi bin Abdillahi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Alisema mtu mmoja, Wallahi -Namuapa Mwenyezi Mungu- hatomsamehe Mwenyezi Mungu fulani, Akasema Mwenyezi Mungu: Ninani anayejiapiza kwangu kuwa sitomsamehe fulani? Hakika mimi nimemsamehe, na nimeyaporomosha matendo yako". Na katika hadithi ya Abuu Huraira: Nikuwa msemaji hapa alikuwa ni mtu mchamungu, Amesema Abuu Huraira: "Alizungumza neno moja lililoteketeza dunia yake na Akhera yake".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහලالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa njia ya kutahadharisha juu ya hatari ya ulimi, kuwa mtu mmoja aliapa kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe mtu mmoja aliyekuwa akitenda madhambi; kana kwamba kamuhukumia Mwenyezi Mungu na kamfungia maamuzi; alipoamini ndani ya nafsi yake kuwa yeye kwa Mwenyezi Mungu ana ubora na thamani na nafasi, na kwa huyu mkosefu ana udhalili, na huku ni kumuelekeza Mwenyezi Mungu na ni utovu wa adabu kwake, akamuwajibishia mtu huyo tabu na hasara Duniani na Akhera.التصنيفات
Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.