Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye

Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye

Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ameeleza bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayepatwa na umasikini" Yaani: shida kubwa, na yamekithiri matumizi ya neno hili katika umasikini na maisha magumu. "Akauteremsha kwa watu" Yaani: Aliweka wazi kwao, na akaidhihirisha kwa njia ya malalamiko kwao, na akataka kuondolewa kwa umasikini wake toka kwao. Hivyo matokeo ni: "Hautozibwa umasikini wake" Yaani: haitokidhiwa haja yake, na hautoondoka umasikini wake, kila inapotatuliwa shida yake inampata shida nyingine zaidi ya hiyo. Na ama "atakayeishusha kwa Mwenyezi Mungu" akategemea kwa Mola wake basi "anakuwa karibu mno Mwenyezi Mungu" Kumpa haraka "kwake riziki ya haraka, yuko karibu kumpa mali na amfanye kuwa tajiri "Au ya baadaye" katika Akhera.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.