kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli

kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli

Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah]

الشرح

Anasema bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ninasema uongo -tukichukulia kutokea hilo- kunapendeka zaidi kwangu kuliko kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ni mkweli ndani yake; na hii nikuwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwa uongo kumeshinda kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli; kwasababu kuapa kwa Mwenyezi Mungu katika hali hii kuna uzuri wa tauhidi, na kuna ubaya wa dhambi la uongo, na kuapa kwa asiyekuwa yeye kwa ukweli, kuna uzuri wa ukweli na dhambi ya ushirikina, na zuri la tauhidi ni kubwa zaidi kuliko zuri la ukweli, na dhambi la uongo ni jepesi sana kuliko dhambi la ushirikina.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.