Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa

Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa

Kutoka kwa Abuu Dharri Al-Ghifaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa pana".

[Sahihi] [Imepokelewa na Abii Shayba katika kitabuchake Al Arshi]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ya Abuu dharri kuwa kursiy pamoja na upana wake na ukubwa wake ukilinganisha na Arshi ni kama bangili la chuma lililowekwa katika jangwa la ardhi pana; Na hii inaonyesha ukubwa na utukufu wa muumbaji wake na uwezo wake uliotimia.

التصنيفات

Kumpwekesha Allah kwa vitendo vyake(Uumbaji)