إعدادات العرض
Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi
Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Portuguêsالشرح
Wametofautiana wanachuoni katika kubainisha maana ya hadithi hii, katika mitazamo mingi: Wa kwanza: Nikuwa makusudio yake: ni wale watu wa zama zake, na maana yake nikuwa atakayemuona usingizini na akawa hakuhama, hajawezeshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhama na kumuona yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa macho wazi. Na ya pili: Nikuwa anayeonekana kwake usingizini ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- halisi, yaani katika ulimwengu wa roho, na kuwa kumuona kwake ni kweli, lakini sharti iwe kwa sifa yake inayojulikana-. Ya tatu: Nikuwa yeye ataona uhakika wa hiyo ndoto akiwa macho akhera; ni kumuona maalumu kwasababu ya kuwa karibu naye na kupata utetezi wake na mfano wa hayo. Kauli yake: "Au ni kana kwamba kaniona akiwa macho" Hii ni riwaya ya Imamu Muslim kaipokea ikiwa na shaka katika mapokezi yake: Je alisema -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ataniona akiwa macho?" au alisema: "Ni kana kwamba kaniona akiwa macho". Na maana yake: nikuwa atakayemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ndoto kwa sifa zake ambazo yeye yuko nazo basi ni kana kwamba kamuona akiwa macho, hii ni kama kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, kama ilivyokuja katika sahihi mbili (yaani kitabu cha sahihi Bukhariy na sahihi Muslim): "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona" na katika riwaya nyingine ndani ya sahihi mbili pia: "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona mimi kweli". kauli yake: "Hajifananishi shetani na mimi", na katika tamko jingine: "Atakayeniota mimi usingizini atakuwa kaniona mimi, kwani hakika haimpasi shetani kujifananisha kwa sura yangu". Na maana yake: nikuwa shetani haiwezekani kwake kujifananisha na Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika umbile lake halisia, na vinginevyo anaweza kuja shetani na akasema kuwa yeye ndiye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na anakuwa katika umbile ambalo si umbile lake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, huyu si Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mtu atakapomuota mtu ndotoni na ikaingia hisia nafsini mwake kuwa huyu ndiye Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-, basi hebu atafute sifa za huyu aliyemuona, je zinaendana na sifa za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake au la? Ikiwa zitaendana: Basi atakuwa kamuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na zisipoendana basi huyo si Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- bali hizi ni dhana toka kwa shetani kaziingiza katika nafsi ya huyu aliyelala kwamba ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wala si yeye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na amepokea Imamu Ahmadi na Tirmidhiy katika shamaail: kutoka kwa Yazidi Al faarisiy amesema: Nilimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, nikasema kumwambia bin Abbas: Hakika mimi nimemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, akasema bin Abbasi: hakika Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Hakika shetani hawezi kujifananisha na mimi, basi atakayeniona mimi usingizini hakika atakuwa kaniona mimi", Je unaweza kueleza sifa za huyo bwana uliyemuota? Nikasema: Ndiyo: alipoeleza sifa zake, akasema bin Abbas: lau kama ungemuona ukiwa macho usingeweza kumsifia juu ya hapo" Na maana yake: nikuwa lau kama ungemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ukiwa macho isingewezekana kumsifia zaidi ya hayo uliyomsifia, na hii maana yake nikuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kweli.التصنيفات
Adabu ya kuona Ndoto