Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu?

Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu?

Kutoka kwa Abii Qatada Haritha bin Ribiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisimama kati yao, akawaeleza kuwa kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumwamini Mweyezi Mungu ndio matendo bora, akasimama bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasi na kurudi nyuma" Kisha akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Umesema vipi?" Akasema: Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasina kurudi nyuma, isipokuwa deni; kwani Jibrili ziwe juu yake Amani kanieleza hivyo mimi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alisimama Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kati ya maswahaba kwaajili ya kuwahutubia, akawaeleza kuwa kupigana jihadi kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu na kumuamini Mwenyezi Mungu ndiyo matendo bora, akasimama bwana mmoja akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hivi unaonaje kama nitauwawa kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu je nitasamehewa mimi madhambi yangu?, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, lakini kwa sharti uwe umeuwawa ukiwa na subira na uvumilivu kwa yale yaliyokupata, ukitakasa nia kwaajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bila kukimbia kiwanja cha vita, kisha akakumbuka Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kitu, nacho ni deni, akakumbusha kuwa jihadi na shahada havifuti haki za wanadamu.

التصنيفات

Fadhila za Jihadi.