Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu

Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu

kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Bilali wakati wa swala ya Alfajiri: "Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Aliona Mtume rehema na amani ziwe juu yake usingizini kuwa yuko Peponi, akasema kumwambia Bilal bin Rabaha: Nieleze kuhusu amali yoyote ya sunna yenye matarajio makubwa uliowahi kuifanya ndani ya Uislamu? kwani mimi nilisikia sauti ya chini ya viatu vyako wakati wa kuvitikisa kwa kutembea mbele yangu Peponi. Bilal akasema: Sikuwahi kufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa yoyote kwangu zaidi yakuwa sijawahi kutengukwa udhu wakati wowote iwe usiku au mchana isipokuwa ninatawadha, kisha ninaswali kwa ajili ya Mola wangu kwa udhu huo swala za sunna zisizo na mpaka kiasi nilichoandikiwa kuswali.

فوائد الحديث

Ubora wa amali aliyoisema Bilal radhi za Allah ziwe juu yake, nayo ni swala kila anapopata twahara na akatia udhu, na kwamba hiyo ni miongoni mwa amali inayotarajiwa zaidi, na ni sababu ya kuingia Peponi.

Sunna ya kuswali baada ya kila udhu.

Kiigizo na mlezi kuuliza matendo ya mwanafunzi wake; ili amhimize kudumu nayo kama ni matendo mazuri, na kama si hivyo basi amkataze.

Ushahidi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Bilal radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ni katika watu wa peponi.

Swali hili lilikuwa wakati wa swala ya Alfajiri, na kwa hili ni ishara kuwa tukio hili lilitokea katika ndoto yake rehema na amani ziwe juu yake, na ndoto za Manabii ni kweli.

التصنيفات

Maisha ya Akhera., Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.