Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka aliteremsha "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri

Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka aliteremsha "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka aliteremsha "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maaida: 44] na "basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "basi hao ndio waovu" [Maida: 47], akasema: Amesema bin Abbasi: Aliziteremsha Mwenyezi Mungu kwa makundi mawili katika Mayahudi, na moja lilikuwa limelitenza nguvu jingine katika zama za ujinga, mpaka wakaridhiana na wakapatana kuwa kila dhalili aliyeuliwa na mtu mtukufu fidia yake ni Waski hamsini, sawa na (kg 6100), na kila maiti aliyeuliwa na mtu dhalili katika watukufu basi fidia yake ni Waski mia moja (100) sawa na (kg12,200), na walikuwa wakiishi katika maisha hayo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mji wa Madina, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati huo hajajulikana kwa watu, na hakuwa amewalazimisha na kuwatenza nguvu katika hilo, na huo ulikuwa ni wakati wa ule mkataba wa maridhiano (Hudaibia), basi mtu dhalili akamuuwa mtukufu mmoja, basi yule mtukufu akatuma ujumbe kwa ndugu wa yule dhalili kuwa tunataka mtuletee Waski mia moja (kg12,200) yule dhalili akasema: Je ni kweli ndivyo ilivyokuwa katika mitaa yao kwamba dini yao ni moja, na nasaba yao ni moja, na mji wao ni mmoja, kwamba fidia ya baadhi yao ni nusu ya wenzao? Bila shaka hakika sisi tumekupeni kiasi hicho kwa kutudhulumu, na kwakuwa tunawaogopa, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni, basi vita ikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muamuzi wao, kisha yule mtukufu akaanza kueleza na akasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni toka kwao zaidi ya kile atakachowapa toka kwenu, na hakika wamesema kweli, hawakutupa isipokuwa kwa dhuluma na kwa kutuogopa sisi, na kuwatenza nguvu, basi tumeni kwa Muhammadi mtu atakayekuleteeni maoni yake: Ikiwa atakupeni mnachotaka basi mfanyeni kuwa hakimu wenu, na asipokupeni basi muepukeni na msimfanye kuwa hakimu, basi wakatuma kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu miongoni mwa wanafiki ili wawaletee habari na maoni ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu alimpa habari Mtume wake ya jambo lao lote na kile walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kuukanusha unabii wako miongoni mwa wanafiki ambao wameonyesha Uislamu..." [Maida: 41] Mpaka katika kauli yake: "Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki (waovu)" [Maida: 47] Kisha akasema kuhusu aya hizo, Wallah zimeteremka, na bila shaka wao ndio Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakusudia.

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Walikuwa miongoni mwa Mayahudi wa Madina ni Bani Kuraidha na Bani Nadhiri, na kabila moja lilikuwa limelitenza nguvu na kulishinda kabila jingine katika zama za ujinga, wakaridhiana na wakapatana kuwa kila mtu aliyeuliwa na mtu mtukufu mwenye nguvu katika madhalili waliozidiwa basi fidia yake ni Waski hamsini tu (kg 6,100), na kila maiti mtukufu aliyeuliwa na mtu dhalili basi fidia yake ni mara mbili, Waski mia moja (kg 12,200) na waski moja ni sawa na vibaba sitini. Walikuwa katika utaratibu huo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuhama, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, naye rehema na amani ziwe juu yake kwa wakati huo alikuwa bado hajapata ushindi dhidi ya maadui zake, na hajawatenza nguvu ili wamtii; kwa sababu hilo lilikuwa mwanzoni mwa kuhama kwake, na ilikuwa kipindi cha mkataba wa maridhiano (Hudaibia). Kabila dhalili mtu mmoja akamuua mmoja katika watu watukufu, kabila tukufu wakatuma ujumbe kwa watu dhalili: Yakuwa tutumieni Waski mia moja kama makubaliano yalivyokuwa tangu awali, kabila dhalili likasema: Je, linawezekanaje hili katika mitaa miwili, dini yao moja, na nasaba yao moja, na mji wao mmoja, halafu fidia ya baadhi yao iwe nusu ya wenzao?!, hakika sisi tulikupeni fidia hii kwa kutudhulumu, na kwa kuwahofu, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni fidia hiyo milele. Vita vikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakimu kati yao, kisha kabila tukufu likatafakari, wakasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni kutoka kwao mara mbili ya kile atakachowapa wao, na hakika wamesema kweli, hawakutupa kiwango hiki isipokuwa kwa dhuluma, na kwa kuwatenza nguvu, tumeni watu kwenda kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa siri watakaokuleteeni mtazamo wake, ikiwa atakupeni mnachokitaka basi mfanyeni kuwa hakimu, na asipokupeni mnachotaka achaneni naye na wala msifanye kuwa hakimu baina yenu. Wakatuma watu kwa siri kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika wanafiki ili wajue mtazamo wake rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Mwenyezi Mungu akateremsha wahyi na akamueleza Mtume wake kuhusu swala lao lote na walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika suratul Maida kwanzia kauli yake: "Ewe Mtume, wasikuhuzunishe wale wanaokwenda mbio katika kukupinga, miongoni mwa wale waliosema tumeamini" [Maida: 41]. Mpaka katika kauli yake: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47]. Kisha akasema bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yao: Kwa makundi hayo mawili Wallahi ndio iliteremka kauli yake Mtukufu: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maida: 44], na "...basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "...basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47], na hao hakika ndio aliowakusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.

فوائد الحديث

Mayahudi walijua ukweli wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na uaminifu wake.

Vitimbi vya Mayahudi na dhuluma zao mpaka hata wao kwa wao.

Habari aliyoitoa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Mayahudi wana fedheha duniani na adhabu chungu Akhera.

Kutohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kuridhika na hukumu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni dalili ya ukafiri na dhulumu na uovu.

Hatari ya wanafiki na kusaidizana kwao na Mayahudi.

التصنيفات

Sababu za kuteremka aya