Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama: Mtu aliyetoa (kiapo) kwa jina langu kisha akafanya usaliti, na mtu aliyemuuza mtu huru kisha akala thamani yake, na mtu aliyempa kazi mwajiriwa, akatimiza majukumu yake na hakumpa malipo yake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Watu wa aina tatu mimi ndiye nitakayepambana nao siku ya Kiyama, na nitakayekuwa mgomvi wake basi nitapambana naye na kumshinda: Wa kwanza: Atakayetoa kiapo na akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na akachukua ahadi kisha akaitengua na kufanya hiana. Wa pili: Atakayemuuza mtu huru kwa kumfanya kuwa mtumwa na akala thamani yake na akakitumia kiwango cha pesa aliyopata. Wa tatu: Atakayemuajiri muajiriwa katika kazi, akamtimizia kazi yake na hakumpa thamani ya kazi yake.

فوائد الحديث

Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake, na huitwa Hadithil-Qudsi au Ilaahi (Hadithi takatifu), nayo ni ile ambayo lafudhi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina umaalumu kama wa Qur'ani ambao imesifika nao, kama kisomo chake kuwa ni ibada, nakuwa na twahara wakati wa kusoma, na kutoa changamoto na mengineyo.

Amesema Assindi: Imesemwa: Kutaja aina tatu haimaanishi ni hizi pekee; kwa sababu yeye Mtukufu ni mpinzani wa madhalimu wote, bali ni kwa ajili ya kuwatilia mkazo watu hawa.

Amesema bin Jauzi: Mtu huru ni mja wa Mwenyezi Mungu, hivyo, atakayemtendea kosa la jinai basi mgomvi wake ni bwana yake, ambaye ni Mwenyezi Mungu.

Amesema Al-Khattwabi: Kumzingatia mtu kuwa yuko huru hutokea kwa mambo mawili: Amuache huru kisha afiche hilo au akane. La pili: Amtumikishe kwa lazima baada ya kumuacha huru , na la kwanza ndio baya zaidi. Nikasema: Na hadithi ya mlango huu iliyoyaeleza ni mabaya mno; kwa sababu pamoja na kuficha kumuacha huru au kukana kuna kutenda kwa muktadha wa hayo, kama kumuuza na kula thamani yake, na ndio maana ahadi ya adhabu ikawa kubwa.